Basata yatoa msimamo wa mwisho sakata la Miss Tanzania

Wednesday November 03 2021
miss tanzaniapic
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limeeleza kuwa hadi sasa wanamtambua Rose Manfere kuwa ndiye mshindi wa taji la Miss Tanzania.

Baraza hilo limeeleza  halitokuwa tayari kukabidhi bendera kwa Mrembo mwingine wasiyemtambua.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Novemba 3, 2021 na Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko alipozungumza na Mwananchi muda mfupi baada ya kukabidhi bendera kwa vikundi vya sanaa za ngoma vinavyokwenda nchini Mayote na Uswiz.

Hivi sasa kamati ya Miss Tanzania inaendelea kumuandaa Miss namba mbili katika mashindano hayo ambaye ni Juliana Rugimisa, ambapo mratibu wake Azama .hivi karibini alisema maandalizi yanaendelea vizuri na mrembo huyo anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu.

Pamoja na mambo mengine leo katika mkutano huo wa kukabidhi vikundi vya ngoma bendera, Mwananchi ilitaka kujua msimamo wa Basata  hadi sasa kuhusiana na sakata hilo ukizingatia ni hivi karibuni Katibu Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi alisema serikali itatoa msimamo wake.

Akilizungumzia hilo, Mniko amesema msimamo wao upo vilevile na ndio msimamo wa serikali na kueleza kuwa hawatakuwa tayari kutoa bendera au kibali kwa Mwakilishi ambaye hawamtumbui kwenda kuiwakilisha nchi.

Advertisement

"Kisheria Rose ndio anayejulikana kama Miss Tanzania 2020/21 na ndio tutampa bendera kwenda Miss World, msimamo ambao hata waandaaji wa mashindano hayo tumewashaandikia barua na wanalijua hilo.

Basata inatoa msimamo huo zikiwa zimebaki siku chache kuelekea mashindando ya Miss World yatakayofanyika Desemba mwaka huu nchini Puerto Rico.

Advertisement