Ben Pol, Arnelisa shauri la kuvunja ndoa yao latua mahakamani

Friday April 30 2021
benpaulpic
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Msanii wa Bongofleva, Ben Pol amethibitisha kufunguliwa kwa shauri la talaka dhidi ya mkewe, Arnelina ambaye ni raia wa Kenya.

Ben Pol aliyefunga ndoa na Arnelisa mwaka 2020 katika kanisa la St Gosper amethibitisha suala hilo leo Ijumaa Aprili 30, 2021 kupitia ukurasa wa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kuibuka madai mtandaoni kuwa wawili hao wametengana.

“Masuala haya ni ya binafsi sana na kwa kuwa shauri linaendelea mahakama ya mwanzo Ben Pol asingependa lizungumzwe zaidi kwa heshima ya pande zote na kwa kuheshimu kazi ya Mahakama,”

“Pia anaomba nafasi na faragha kwake na kwa familia katika kipindi hiki kigumu na anawashukuru wote kwa uelewa na pia kwa familia, marafiki na mashabiki wote kwa sapoti  mnayoendelea kuionesha,” alieleza Ben Pol katika ujumbe huo wenye kichwa cha habari ‘shauri la talaka’ unaoonyesha kuwekwa na uongozi unaomsimamia shughuli zake za muziki.Advertisement


Advertisement