Bi Sonia kuzikwa kesho Uzini Zanzibar

Thursday July 21 2022
maziko pic
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Maziko ya msanii wa filamu Farida Sabu'Bi Sonia' aliyefariki dunia leo Julai 21, 2022 kufanyika  kesho kijijini Uzini, Zanzibar.

Bi Sonia aliyewahi kutamba kwenye filamu mbalimbali ikiwemo, Sikitiko langu, Dengerous Disire amefariki leo asubuhi visiwani Zanzibar ambapo alikwenda kwa ajili ya matibabu mwezi mmoja uliopita.


Mwenyekiti Chama cha WIgizaji, Chiki Mchoma alithibitisha taarifa ya kifo hicho.


Chiki anesema maziko hayo yatafanyika saa 7  baada ya swala ya Ijumaa na msiba upo nyumbani kwa mtoto wake huko Uzini.


Mbali na filamu pia Bi Sonia alikuwa akionekana kwenye filamu ya Kapuni inayoonyeshwa DStv na ile ya Ndoano inayoonyeshwa kituo cha Azam.

Advertisement