Burna Boy awavimbia BET kimtindo

Burna Boy awavimbia BET kimtindo

Muktasari:

  • Ikiwa leo ni siku ya tatu tangu msanii kutokea Nigeria, Burna Boy kushinda tuzo ya BET 2021, hajachapisha chochote kwenye ukurasa wake wa Instagram hata kushukuru kwa ajili ya ushindi huu.

Ikiwa leo ni siku ya tatu tangu msanii kutokea Nigeria, Burna Boy kushinda tuzo ya BET 2021, hajachapisha chochote kwenye ukurasa wake wa Instagram hata kushukuru kwa ajili ya ushindi huu.

Burna Boy alishinda katika kipengele cha Best International Act ambacho aliwakuwa anawania na wenzake kama Diamond Platnumz, Wizkid, Emicida, Headie, Aya Nakamura, Youssoupha na Young T & Bugsey.

Tuzo huzo zilitolea alfajiri ya kuamkia Juni 28, 2021 kwa saa za Afrika Mashariki katika ukumbi wa Microsoft Theater huko Los Angeles nchini Marekani.

Hadi leo Juni 30, 2021 saa nne asubuhi, Burna Boy ameukalia kimya ushindi huo ambao ni wa tatu kwake, pia hajawahi kutoa chapisho lolote kuhusu tuzo hizo hata pale alipotangazwa kuwania tuzo hiyo.

Hii ni tofauti na Diamond ambaye alishukuru kuteuliwa, aliomba mashabiki kumuunga mkono katika tuzo, alichapisha picha akiwa red carper ya tuzo na alishukuru hata pale alipokosa.

Burna Boy ambaye ana wafuasi (followers) milioni 7 Instagram, sio msanii wa makeke mengi kwenye mtandao licha ya ukubwa wa muziki wake duniani hadi kushinda tuzo ya Grammy Machi 14, 2021.