Burna Boy na Diddy kuja na kazi nyingine

Burna Boy na Diddy kuja na kazi nyingine

Muktasari:

  • Msanii kutoka nchini Nigeria, Burna Boy anatarajia kuachia albamu yake ya sita baada ya kupata mafanikio makubwa na albamu ya ‘Twice as Tall’.

Msanii kutoka nchini Nigeria, Burna Boy anatarajia kuachia albamu yake ya sita baada ya kupata mafanikio makubwa na albamu ya ‘Twice as Tall’.

Machi 14, 2021 huko Los Angeles nchini Marekani, Burna Boy alishinda tuzo ya Grammy kupitia 'Twice as Tall' katika kipengele cha albamu bora ya muziki.

Albamu hiyo Mtayarishaji Mkuu  (Executive Producer) alikuwa Sean Love Combs maarufu kama Diddy kutoka Marekani.

Nyota huyo baada  ya kushinda tuzo nyingine ya BET 2021 kama Best International Act, Burna Boy ametangaza kuwa Agosti 14, 2021 ataachia albamu nyingine ambayo Diddy ataisimamia pia.

Utakumbuka albamu yake ya nne, ‘African Giant’ iliyotoka Julai 2019 ilishinda tuzo ya All Africa Music Awards (AFRIMA) kama albamu bora ya mwaka 2019, pia ilichaguliwa kuwania tuzo za 62 za Grammy ingawa haikushinda.