Cpwa kuzikwa saa 10 jioni

Sunday January 17 2021
cpwaa kuzikwa pic
By Kelvin Kagambo

Dar. Mwili wa msanii wa muziki kizazi kipya  Ilunga Khalifa 'Cpwaa' utazikwa leo saa 10 jioni jijini Dar es Salaam.

Akitoa utaratibu wa mazishi, kaka mdogo wa msanii huyo ambaye alikuwa akimuuguza kipindi chote cha maradhi, Murad Omar Khamis amesema kaka yake atazikwa Magomeni jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Mwinyimkuu.

"Kaka tutampuzisha leo leo saa 10 katika makaburi ya Mwinyimkuu. Tunasubiri mwili wake ufike kutoka hospitali,” alieleza.

Akielezea kilichopelekea kifo cha msanii huyo, Murad amesema kaka yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (pnemounia) kwa wiki sasa lakini alizidiwa wiki hii na walimkimbiza hospitali ambapo alilazwa kabla ya umauti kumfika usiku wa kuamkia leo Januari 17.

"Alikuwa anaumwa wiki mbili zilizopita, na akaja kuishi hapa nyumbani kwa mama yake. Ila Jumatano alizidiwa ndio tukamkimbiza hospitali muhimbili, alilazwa ICU," aliongeza. 

Msiba wa Cpwaa uko Magomeni Usalama nyumbani kwa mama yake mzazi, na tayari majirani, ndugu na jamaa wameanza kufika eneo la msiba.

Advertisement
Advertisement