Diamond achaguliwa kuwania tuzo za MTV EMA 2021

Thursday October 21 2021
diamondpic

Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz

By Peter Akaro

Dar es Salaam. Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amechaguliwa kuwani tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) 2021 katika kipengele cha Best African Act.

Katika kipengele hicho Diamond atachuana na wakali wengine Afrika kama Wizkid (Nigeria), Tems (Nigeria), Amaarae (Ghana) na Focalistic (Afrika Kusini).

Licha ya waandajili (MTV EMA) kuweka wazi tuzo hizo zitatolewa Novemba 14, 2021 bado hawajaweka wazi hafla ya utolewaji wake itafanyika wapi.

Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni Diamond kutajwa kuwania tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA) na African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA), kote anawania vipengele zaidi ya vitatu.

Utakumbuka wiki iliyopita Diamond alifanikiwa kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka Afrika (African Artiste of The Year) kutoka Ghana Music Awards UK.

Diamond alikuwa anawania kipengele hicho na wakali wengine Afrika kama Burna Boy, Davido, Wizkid, Master KG, Fireboy, Patoranking, Sinach, Mercy Chinwo, Judikay na Teni.

Advertisement
Advertisement