Diamond aikosa tuzo ya MTV EMA 2021, Wizkid atakata

Monday November 15 2021
wikizipic
By Peter Akaro

Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameshindwa kutakata katika tuzo za MTV Europe Music Awards  (MTV EMA) 2021 zilizotolewa usiku wa kuamkia leo.

Tuzo hizo zilitolea katika ukumbi wa Budapest Sportarena huko Hungary, ushindi umeenda kwa Wizkid wa Nigeria ambaye alikuwa anawania kipengele cha Best African Act.

Ukiachana na Diamond, wasanii wengine waliokuwepo katika kipengele hicho ni Tems (Nigeria), Amaarae (Ghana) na Focalistic (Afrika Kusini).

Katika hatua nyingine, Rayvanny ameandikisha rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kutumbuiza katika katika tuzo hizo ambapo ameshirikiana na Maluma toka Colombia na kuimba pamoja wimbo wao mpya, Mama Tetema ambao Rayvanny kashirikishwa. 

Advertisement