Diamond aingia studio na Busta Ryhmes huko Marekani

Diamond aingia studio na Busta Ryhmes huko Marekani

Muktasari:

  • Msanii wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameingia studio kurekodi wimbo na msanii mkongwe wa Marekani, Busta Ryhmes.


Msanii wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameingia studio kurekodi wimbo na msanii mkongwe wa Marekani, Busta Ryhmes.

Diamond yupo nchini humo toka wiki iliyopita alipohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za BET 2021 ambapo alikuwa anawania kipengele cha Best International Act ambapo msanii kutoka pande za Afrika Magharibi Burna Boy aliibuka kidedea.

Wawili hao wanafanya wimbo huo chini ya mtayarishaji  mkubwa duniani, Swizz Beatz ambaye ni mara ya pili sasa anafanya kazi na Diamond.

Mwaka jana Diamond alishirikishwa na Alicia Keys katika wimbo wake uitwao ‘Wasted Energy’ ambao unapatikana kwenye albamu yake 'ALICIA' ambayo ilifanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard upande wa ‘Top R&B Albums’.

Wimbo huo pia ulitengezwa na Swizz Beatz ambaye ni mume wa Alicia Keys. 


Ukiachana na Alicia Keys, Diamond amefanikiwa kufanya kolabo na wasanii wengine wa Marekani kama Rick Ross, Omario na Ne-Yo.


Kwa sasa mwimbaji huyo yupo katika maandalizi ya albamu yake mpya ya nne baada ya kuachia ‘Kamwambie’ (2010), ‘Lala Salama’ (2012) na ‘A Boy From Tandale’ (2017).