Fally Ipupa amtaja Barnaba

Thursday October 07 2021
ipupapic
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kongo, Fally Ipupa amemtaja Barnaba kuwa ni msanii anayemkubali nchini Tanzania.

Mwanamuziki huyo ameyasema hayo leo Alhamisi Oktoba 7, 2021 alipotua nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya maonyesho yake katika mikoa miwili ya Dar es Salaam na Mwanza.

"Ni kweli nafuatilia sana muziki wa Tanzania na wasanii wote wanaofanya vizuri mimi nawapenda akiwemo Diamond, Alikiba na huyu mwingine anayeimba na kupiga gitaa,nani huyuu...ndio Barnaba," amesema Fally Ipupa.

Akizungumza na Mwananchi, Barnaba amesema anasikia faraja anapotajwa na msanii mkubwa.

"Fally IPupa ni kaka yangu, najisikia faraja kunitaja kuwa moja ya wasanii anaowakubali nami pia namkubali sana kwani huyu ni alama ya muziki wa Afrika, tuna kila sababu ya kujivunia kuwa naye" amesema Barnaba.

Hata hivyo amesema amefahamiana na msanii huyo siku nyingi tangu alipokuja Tanzania miaka kumi iliyopita licha ya kuwa hawajawahi kuimba naye wimbo wa pamoja.

Advertisement

Fally Ipupa ni kati ya wasanii wa Kongo waliofanya kolabo na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na kupokelewa vizuri kwenye soko ambaye amemshirikisha katika wimbo wake' Inama'.


Advertisement