Fally Ipupa kufanya kolabo nyingine na mwanamuziki wa Tanzania

Tuesday October 12 2021
Kolabo pc
By Mgongo Kaitira

Mwanza. Ukiachana na Kolabo maarufu ya ‘Inama’ aliyofanya msanii wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Fally Ipupa na Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz,’ msanii huyo amesema Watanzania wakae mkao wa kula kwani hivi karibuni atatoa   wimbo mwingine na msanii kutoka Tanzania.

Akizungumza leo Oktoba 12, ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika shoo yake jijini hapa, Meneja wa msanii huyo Madina Djobongue amesema Fally Ipupa anaendelea kufatilia ni msanii gani afanye naye kolabo kabla ya kuondoka nchini.

Djobongue ametaja baadhi ya wana muziki ambao Fally Ipupa anawakubali kuwa ni pamoja na Ali Kiba, Barnaba na Diamond Platinumz.

"Bongofleva ni muziki unaoonesha asili ya muafrika ndiyo maana Fally yuko tayari kufanya kolabo na msanii kutoka nchini Tanzania, yuko tayari kusikiliza wimbo kutoka kwa msanii yoyote ikitokea ameukubali basi hana shida ataingiza sauti ndani ya hata dakika mbili," amesema Djobongue.

Ameongeza kwamba baada ya msanii huyo kumaliza shoo yake jijini Mwanza atatembelea vivutio vya utalii nchini ili kuutangaza utalii wa Tanzania.

"Wakazi wa Kanda ya Ziwa wajitokeze kwa wingi hapa ilipo hoteli ya Malaika tunaamini hawatojutia kutoa kiingilio chao," amesema Djobongue

Advertisement
Advertisement