Gigy Money: Sijui na mimi nitafunguliwa

Tuesday April 06 2021
GIGY PIC
By Nasra Abdallah

Baada ya Rais Samia Hassan Suluhu kuagiza kufunguliwa kwa vyombo mbalimbali vya habari vilivyofungiwa, Gigy naye aamka na ombi lake.

Rais Samia leo Jumatatu Aprili 6, 2021 akiwa anawaapisha  makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu wa wizara na wakuu wa taasisi mbalimbali  katika moja ya mambo aliyoyazungumzia ni kuagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyofungiwa.

Saa chache baada ya agizo hilo, Gigy ambaye jina lake halisi ni Gift Stanford, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameandika” Sijui na mimi nitafunguliwa,”

Januari 5, 2021, Basata ilitangaza kumfungia miezi sita msanii huyo kutojihusisha na kazi za sanaa ndani na nje ya nchi.

Basata ilisema ilifikia hatua hiyo baada ya Gigy akiwa katika tamasha la ‘Tumewasha Tour’, jijini Dodoma kuvua nguo na kubaki na vazi lilionyesha maungo yake ya mwili.

Walibainisha kuwa kitendo hicho kilidhalilisha utu wa msanii huyo na kubughudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya nchi.

Advertisement
Advertisement