Harmonize ampa moyo Kajala

Monday February 15 2021
Harmonize pic
By Nasra Abdallah

Ikiwa imepita siku moja baada ya kuvuja kwa video  chafu ya mtoto wa msanii Kajala Masanja, anayefahamika kwa jina  la Paula, Harmonize ampa moyo msanii huyo.
Kajala ambaye ni msanii wa filamu, tunaweza sema jana Jumapili Februari 14, 2021 Valentine yake iliingia doa baada ya picha hizo mbaya kuvuja na kugeuka kuwa gumzo huko mtandaoni.
Video hiyo inamuonyesha mtoto huyo wa Kajala akiwa kwenye gari na msanii kutoka lebo ya WCB, Rayvanny wakiwa katika mahaba mazito.
Licha ya mwenyewe kuelekeza tuhuma za aliyesababisha hayo yote  kuwa ni mrembo Hamisa Mobeto, Mobeto naye amechomoa kwa kuandika utetezi mrefu kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.
Hata hivyo katika siku hiyo ya wapendanoa ni kama Harmonize amempa moyo kwa magumu anayoyapitia mpenzi wake huyo kwa kumuandikia ujumbe mtamo wa mapenzi.
Kupitia ukurasa wake Harmonize ameandika’ Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu wa maisha, kuwa imara, unanifanya nijivune,”
Hali ilivyokuwa
Baada ya kusambaa kwa video hiyo, Kajala alijitokeza na kuandika ujumbe mrefu wa kumlaumu Mobeto kuwa ndio sababu kwa kile alichoeleza siku tukio Mobeto alikuwa kamtoa out mtoto wake huyo kipenzi.
Kajala alienda mbali na kueleza kuwa Rayvanny na Mobeto walemnywesha  pombe mtoto wake ili kutimiza malengo yao na  kujikuta anafanya mambo hayo ya ajabu.
Shutuma hizo zinamuibua Mobeto kuzijibu na kuweka ushahidi wa video  kuwa siku anayoelezwa kuwa alitoka na mtoto huyo hakuwa na aina ya nywele za bandia alizobandika  kama anavyoonekana akiwa na Rayvanny, nakuomba watu kuacha kumfanya jumba bovu kila takataka kurushiwa.
Katika sakata hilo aliomba alaumiwe  kwa kumtoa out ambapo hata hivyo alikuwa akiwasiliana na mama yake nyakati zote lizokuwa nazo mpka pale alipomrudisha kwake, lakini sio kwa video hiyo ambaye anaeleza kutohusika kushiriki kwa namna yeyote ile.
Tayari  Hamisa ameeleza kuchukua hatua zaidi kupitia mwanasheria wake kwa kile alichodai kuchafuliwa huku Kajala yeye akiomba mamlaka kumsaidia kwa kitendo alichofanyiwa mtoto wake.

Advertisement