Harmonize amwibukia Raynavy mtandaoni

Monday February 15 2021
Rayvany pi
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mzozo wa kuvuja kwa video chafu ya Paula ambaye ni mtoto wa msanii wa filamu, Kajala Masanja  unaendelea na sasa msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajab Kahali maarufu kama Harmonize naye amefunguka.
Video hiyo iliyovuja jana Jumapili, Februari 14,2012 ambapo kajala amemhusisha msanii mwenzake Hamisa Mobeto akidai kuwa alitoka na manaye muda mfupi kabla ya kupiga picha hizo akiomba mamlaka Serikali kuingilia kati.  
Hata hivyo, Mobeto ameyakanusha madai hayo na kutishia kuchukua hatua za kisheria.
Wakati tukio hilo likitokea, Kajala alikuwa akijirusha na msanii Harmonize na picha zao zilisambaa mitandaoni. Leo msaanii huyo aliyejitoa kundi la Wasafi Classic ameandika katika ukurasa wake wa Instagram akimwonya msanii mwenzake Raynavy aliyepiga picha na Paula mtoto wa Kajala.  
Ukiachilia Hamisa na Kajala, sasa msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul maarufu kwa jina la Harmonize ametia neno katika sakata hilo huku akieleza huenda kosa ni yeye kuingia kwenye mahusiano na Kajala.
"Ray my Brother yafuatayo sitoyasema Kama Mimi ni mzazi wa Paula ndiyo naandika kama mzazi niliye na mtoto wa kike (Zurekha). Lakini Pia Kama msani mwenzio, najiuliza tuu..!! Ulipata wapi ujasiri huu wa Kutembea na mwanafunzi Wa kidato cha (5) wakati ni wazi ya kwamba ni kosa la jinai?” amehoji Harmonize.
Ameendelea; "Hukumu yake siyo chini Ya miaka 30. Pia Isitoshe una record na video ukiwa una kiss (busu) yaani unaonyesha kwamba Serikali haiwezi kukufanya kitu.
"Nawaza lengo lilikuwa ni kuonyesha kwamba upo juu ya sheria ? Hebu angalia future(mustakabali) wa mtoto wawatu umeiweka wapi wa tamaa za siku moja. Kama kweli mlikuwa mnapendana mko katika mapenzi video likuwa na Haja Gani And Lengo La Kuvujisha nini ...??
Harmonize katika ujumbe huo ameenda mbali zaidi  na kusema "Kama Tatizo lilikuwa ni mimi Kumpenda mama yake na watu wengi wakavutiwa na sisi si ungetafuta mkubwa mwenzio.”

Advertisement