Harmonize athibitisha kuachana na Anjella, akana kumdai

Muktasari:

Bosi wa lebo ya Konde Music, Rajab Abdul ‘Harmonize’ leo Jumamosi Novemba 5, 2022 amethibitisha taarifa za kuachana na msanii wake Angelina Samson ‘Anjella’


Dar es Salaam. Bosi wa lebo ya Konde Music, Rajab Abdul ‘Harmonize’ leo Jumamosi Novemba 5, 2022 amethibitisha taarifa za kuachana na msanii wake Angelina Samson ‘Anjella’

Angela alitambulishwa kwenye lebo hiyo Machi 11, 2021 ambapo aliachia wimbo ‘Kama’ aliomshirikisha Harmonize na mpaka sasa wimbo huo umeshatazamwa zaidi ya mara milioni tatu kwenye mtandao wa Youtube.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Harmonize ameandika “nilikutana na Anjella akiwa amejikatia tamaa akiwa na ndoto kichwani, sikujiangalia nina kiasi gani, niliamini kwa kuwa watu wapo wananisapoti bila kuwalipa senti tano basi watasapoti kipaji cha dada Anjella.

“Nilichoangalia ni ndoto hasa za mtoto wa kike, nimejitahidi kufanya ya uwezo wangu najua kuna wenye uwezo mkubwa kunizidi.

“Ukizingatia nimeanza juzi kama kuna anayeweza kumuendelezea kipaji chake ni faraja kwangu asisite kujitokeza, puuzia siasa zakusema sijui namdai hela sijawahi kumdai hata senti,”ameandika Harmonize.

Hivi karibuni Harmonize pia amemalizana na wasanii wake wawili Cheed na Killy baada ya wasanii hao kufikisha madai yao katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).