Harmonize ‘kuhamia’ Marekani

Friday July 09 2021
harmonizepic
By Peter Akaro

Dar es Salaam. Msanii wa Bongofleva kutoka Konde Music Worldwide, Harmonize anatarajia kufanya ziara ya kimuziki kwa muda wa miezi miwili nchini Marekani kuanzia Agosti 15, 2021.

Msanii huyo  atafanya shoo ya kwanza Agosti 28, 2021 katika jimbo la Ohio. Harmonize ameeleza kuwa  hivi karibuni atatoa ratiba nzima ya ziara yake hiyo ya kwanza kwa mwaka 2021 nje ya nchi.

Msanii mwingine wa Bongofleva, Diamond Platnumz yupo nchini humo wiki ya pili sasa, tangu alipohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za BET 2021.

Mbali na Harmonize msanii mwingine wa Nigeria, Wizkid naye alitoa ratiba ya shoo zake  zitakazoanza rasmi Septemba 10, 2021 hadi Januari 22, 2022  nchini Marekani.

Baadhi ya maeneo ambayo Wizkid atakafanya shoo ni Boston, MA, Chicago, Minneapolis, Las Vegas, Houston na Dallas.


Advertisement
Advertisement