Huduma Basata, Cosota na Bodi sasa kiganjani

Tuesday November 23 2021
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Serikali imezindua mfumo wa huduma ya kidigitali kwa ajili ya taasisi zinazosimamia sanaa nchini.

Taasisi hizo ni Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),Taasisi ya Haki Miliki Tanzania(Cosota) na Bodi ya filamu.

Mfumo huo ulizinduliwa jana Novemba 22,2021  na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wizara hiyo na wasanii.

Bashungwa amesema mfumo huo utarahisisha kazi kwani wataweza kupata huduma za taasisi hizo popote walipo.

"Mfumo huu wa kidigitali ni mzuri, ninachoomba kwa taasisi husika kuendelea kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wasanii mpaka hapo watakapoelewa kuitumia mifumo hiyo," amesema Waziri Bashungwa.

Kwa nyakati tofauti wakielezea mfumo huo akiwemo Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko amesema kupitia mfumo huo ukiachilia mbali wasanii kujisajili, pia wataweza kupata vibali vya kwenda kufanya show nje ya nchi.

Advertisement

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dk Kiagho Kilonzo amesema kupitia mfumo wasanii wataweza kupata vibali vya kutengeneza filamu ndani ya siku moja badala ya siku 30.

Advertisement