James Bond aja na 'No Time, to Wait', anayemuigiza kustaafu

Wednesday September 29 2021
jemsibondipicc
By Mwandishi Wetu

London, Uingereza (AFP). Watu maarufu na kutoka familia ya kifalme watapita juu ya zuria jekundu jijini London jana Jumanne Septemba 28, 2021 kwenda kushuhudia uzinduzi uliosubiriwa kwa muda mrefu wa filamu ya "No Time To Die" ambayo muhusika mkuu ni James Bond.

Filamu hiyo ya tano na ya mwisho kwa Muingereza Daniel Craig kuigiza kama James Bond, iliahirishwa mara kadhaa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.

Filamu hiyo itaonyeshwa kwenye ukumbi wa kihistoria wa Royal Albert jijini London, huku watoto wa malkia na wake zao, Charles na Camilla na Prince William na Kate wakitarajiwa kuhudhuria.

Filamu hiyo itahamia katika kumbi nyingine nchini Uingereza Alhamisi na nchini Marekani Oktoba 8 -- ikiwa ni mwaka mmoja na nusu baada ya muda uliopangwa.

Filamu hiyo ni sehemu ya sinema nyingine kubwa zilizozuiwa na wasambazaji wakati wa mlipuko wa corona, ambao uliathiri sinema kwa kiwango kikubwa.

Katika filamu hiyo, ambayo imegharimu dola 250 milioni, Bond anarejea katika utumishi baada ya kustaafu, akiahidi: "Lazima nimalize hili."

Advertisement

Anatumia vifaa vyake vyenye teknolojia ya hali ya juu katika maeneo aliyoigizia nchini Italia na Norway, akipambana na mabaya ya Safin, nafasi iliyoigizwa na mshindi wa tuzo za Oscar, Rami Malek (filamu ya "Bohemian Rhapsody").

"Napigwa risasi na baadaye nalipuliwa. Napata hisia za James Bond," Craig alisema.

Huku Craig akielekea kustaafu, ubashiri unazidi kuhusu mtu atayerithi kuigiza nafasi ya James Bond.

Wabashiri nchini Uingereza wanawapa nafasi wasanii wawili; Tom Hardy, aliyeigiza filamu za "The Revenant" na "Dunkirk" au Rege-Jean Page, nyota chotara wa filamu ya "Brudgerton" inayotamba Netflix.

Craig ameigiza kama James Bond kwa kipindi kirefu kulinganisha na waliomtangulia, akianzia mwaka 2006 katika filamu ya "Casino Royale".

Advertisement