John Legend, Mary J Blige, Reznor watajwa tuzo za Oscar

Wednesday February 10 2021
burudani pic

John Legend

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Nyota kadhaa wa muziki duniani wameingia katika kinyang'anyiro cha tuzo za filamu za Oscars zitakazofanyika Aprili 25 baada ya orodha ya filamu zinazowania tuzo kutangazwa jana.

Trent Reznor na Atticus Ross wametajwa kuwania tuzo mara mbili kutokana na kazi yao katika filamu ya Mank na kolabo yao pamoja na Jon Batiste katika filamu ya "Soul".

Kwa mujibu wa tovuti ya Oscar iliyotangaza wanaowania tuzo tisa za awali, nyimbo za wawili hao zinawania tuzo ya Original Score, ambayo hutolewa kwa wimbo bora ulioandikwa maalum kwa ajili ya filamu.

Nyota wengine katika tuzo za Oscar ni Janelle Monáe ambaye kibao chake cha “Turntables” kiko katika filamu ya All In: The Fight for Democracy inayowania tuzo ya Original Song, ambayo hutolewa kwa waandishi bora wa wimbo ulioandikwa maalum ajili ya filamu.

Janelle Monáe

Janelle Monáe

Mwingine ni mwanamama Mary J. Blige na wimbo wake wa “See What You’ve Done” ulio katika filamu ya Belly of the Beast.

Advertisement
marjbridepic

Mary J. Blige

Pia yumo Sacha Baron Cohen na wimbo wake wa “Wuhan Flu” (Delivery of Prodigious Bribe to American Regime for Make Benefit Once Glorious Nation of Kazakhstan)

Nyota wa R&B, John Legend ameingiza wimbo wake wa “Never Break” ulio katika filamu ya Giving Voice, wakati Forest Whitaker na Anika Noni Rose wanawania tuzo hiyo kutokana na wimbo wao wa “Make It Work” katika filamu ya A Christmas Journey.

burudani pic

John Legend

Mwanamuziki machachari, Christina Aguilera anawania tuzo hiyo ya Original Song na wimbo wake wa “Loyal Brave True” unaosikika katika filamu ya Mulan.

Christina Aguilera

Christina Aguilera

Legend na Diane Warren pia wametajwa katika kuwania tuzo mbili katika filamu za Giving Voice na Jingle Jangle: A Christmas Journey, na Warren anawania tuzo kutokana na filamu za The Life Ahead na The One and Only Ivan.

Diane Warren

Diane Warren

Legend alishawahi kushinda tuzo ya Oscar kutokana na wimbo wake wa "Glory" kuwa katika filamu ya Selma.

Kwa mujibu wa sheria mpya za Oscar, filamu zilizoanzia katika huduma za mitandao, sasa zinaweza kuingizwa kuwania tuzo. Sharti la tuzo za Original Score linaruhusu muziki ambao angalau asilimia 60 ni mpya.


Advertisement