Kajala na Mobeto wapandiana mitandani

Sunday February 14 2021
Kajala, Mobetto pic
By Anna Potinus

Umezuka mtafaruko wa aina yake kati ya warembo na wasanii wa maigizo, Kajala Masanja na Hamisa Mobetto baada ya wawili hao kurushiana maneno katika mitandao ya kijamii kutokana na kusambaa kwa video ya mtoto wa Kajala, Paulah akionekana akiwa katika mazingira ya mahaba na msanii wa muzuiki wa kizazi kipya (jina linahifadhiwa).
Video hizo zilizoanza kusambaa mapema leo Jumapili Februari 14, ambapo Kajala amemtuhumu Mobeto kuhusika. Hata hivyo, Mobeto amekanusha madai hayo akisema alikwenda naye kwenye chakula cha mchana na siyo vinginevyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kajala aliweka ujumbe mrefu akitoa malalamiko kwa hamisa kuwa alimuomba atoke na mwanaye kwa ajili ya chakula cha mchana lakini badala yake alienda kumlewesha kwa manufaa yake binafsi huku akiomba Serikali imsaidie kuingilia kati suala hilo kwani mtoto wake bado ni mdogo kitendo kile kinaweza kumuharibia ndoto zake.
“Mimi ni mzazi ambaye ninamlea mtoto wangu kwa katika mazingira magumu kutokana na tofauti moja mbili tatu na baba mtoto wang. Nilikuwa nikipambana na kumpa kila anachotaka mtoto wangu ili aweze kutimiza ndoto zake kama msichana mana kesho nitakuja kumtegemea.
“Shutuma nyingine huwa zinanijia mimi moja kwa moja kama mzazi wa Paula sina budi ya kuzipokea na kukumbana nazo kwani Mungu anajua ukweli wangu,” ameandika Kajala katika mtandao wa Instagram
Amedai kuwa kuwa Februari 9, saa 6 mchana, Hamisa Mobeto alimwomba atoke na mwanaye wakapate chakula cha mchana na alimkubalia.
“Kumbe ndo hiyo siku alitake advantage kwenda kumkutanisha na (anamtaja msanii) kwa manufaa yake binafsi. Walimrubuni mtoto mdogo kwa kumnywesha pombe, wamemrecord video chafu. Sawa mimi ni Mnyonge siwezi wafanya chochote basi hata muogopeni Mungu na kama Mungu hamumwoni Hamuiogopi serikali?” amehoji Kajala.  
Hata hivyo, Mobeto naye amejibu tuhuma hizo katika ukurasa wake wa Instagram amesema alichokifanya ni kumpeleka mtoto huyo kwenye chakula cha mchana na kwamba wakati anatoka naye hakuwa amesuka nywele anazoonekana nazo katika video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii.
Pia amesema baada ya kumaliza kula alimrudisha binti huyo kwa mama yake hivyo taarifa zote ni za uongo huku akimuonya Kajala kuacha kumchafulia jina lake mitandaoni.
“Jamani hata kama Hamisa Mobetto ndio jumba bovu lenu la kutupia takataka ifike mahala ifike ukomo. Siamini kama baada ya kukaa na kutafakari cha kueleza haya mmeona mimi ndio ninaweza kuwa Damage Controller (wa kudhibiti uharibifu).

“Nilimtoa Lunch na muda wote nilikua naongea na wewe kwenye simu mpaka nimemrudisha hapo Gym kwako Mimi mwenyewe soon after lunch.
“Hauoni Kama unaongea uongo hadharani bila woga? Siku ninatoka na Paula alikuwa na nywele hizo za kwenye videos? Naomba nilaumiwe kwa kukubali ombi la kumpeleka mwanao lunch na si vinginevyo. Mimi ni mama, mfanya biashara, mdau na balozi wa makampuni mbali mbali. Brand (jina la biashara) yangu nimeijenga kwa muda mrefu hivyo ningependa iheshimike na isichafuliwe kwa shutuma za uongo kama hizi,” ameeleza Mobeto.

Advertisement