Kamati ya vazi la Taifa kuanzia hapa...

Sunday July 24 2022
kamatipic
By Peter Akaro

Zikiwa zimepita siku mbili baada ya kuteuliwa kwa kamati mpya ya kusaka vazi la Taifa na ya kuratibu mchakato huo, imeelezwa wataendelea ilipoishia kamati ya awali.

Baada ya kutangazwa kamati hiyo mpya ulizuka mjadala kuwa inakwenda kutumia vibaya fedha za Serikali kwa sababu kazi hiyo ilishaanza na mchakato kuishia njiani.

Hata hivyo akilifafanua hilo katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo,Mohammed Mchengerwa,alisema kamati hiyo itaanzia ilipoishia ya awali iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Joseph Kusaga ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Cloud Media.

Hatua hiyo inakuja ikiwa zimepita zaidi ya wiki mbili tangu Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa alipotoa maagizo ya kuendelea kwa mchakato wa kupatikana kwa vazi hilo.

Ukiachana na Kusaga katika kamati ya awali iliyoundwa mwaka 2014, Katibu alikuwa Angela Ngowi huku wajumbe wa kamati hiyo wakiwa ni Habib Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Makwaia Kuhenga, Ndesambuka Merinyo na Absalom Kibanda, ambaye baadaye alitangaza kujiweka kando.

Wakati kamati mpya inayoanza mchakato huo sasa ipo chini ya uenyekiti wa Profesa Hermas Mwansoko ambaye ni Mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, huku Katibu akiwa Dk Emmanuel Temu, Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni.

Advertisement

Wajumbe wengine waliotajwa na wanapotokea kwenye mabano,Chifu Antonia Sangali(mwakilishi wa Machifu),Hadija Mwanamboka(mbunifu mitindo),Mustafa Hasanali(mbunifu mitindo),Mrisho Mpoto(Msanii na Masoud Ally maarufu kwa jina la Kipanya(msanii wa uchoraji na usanifu).


Mchakato wa awali ulivyoanza na kukwama

Mchakato wa kutafuta vazi la Taifa ulianza mwaka 2004 ambapo kuliundwa kamati maalum na aliyekuwa Waziri wa Habari,Sanaa Utamaduni na Michezo wakati huo Dk Emmanuel Nchimbi.

Hata hivyo baada ya kutokea mabadiliko katika baraza la Mawaziri mwaka 2011 ambapo Fenera Mkandala alikabidhiwa kusimamia Wizara hiyo ,kamati maalum iliyeteuliwa kulisimamia upatikanaji wa vazi hilo ilikabidhi michoro sita kwa Waziri huyo kwa ajili ya vazi hilo waliyoipata katika michoro 200 waliopelekewa na wasanii mbalimbali, lakini hakuna kilichoendelea hadi sasa.

kwa sababu hawezi kutumbuiza bila kuwa na wachezaji ambao anatakiwa kuwalipa na gharama za maandalizi.

Kundi hili linaloundwa na wasanii wawili wao wamesema chini ya Sh10 milioni hawapandi jukwaani kabisa kutokana na ukubwa muziki wao kwa sasa katika soko, ila itategemea na aina ya shoo. Mbali na hiyo ikiwa ni shoo ya mkoani, yaani nje ya Dar es Salaam, basi waandaaji wanapaswa kuwakatia tiketi tano za ndege ambazo mbili za kwao, tatu za meneja, mpiga picha na mlinzi au prodyuza wao.


Maoni ya wabunifu

Awali akichangia kuanza kutekelezwa kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, mbunifu wa mavazi wa siku nyingi Hadija Mwanamboka, anasema “Kamati imeteuliwa nikiwamo, ina Mwenyekiti na sisi wajumbe kauli ya waziri ni maelekezo bila shaka tutakutana na kujadili kwa pamoja nini kifanyike, lengo ni kusonga mbele kwa mafanikio.


Tamwa watoa neno

Hata hivyo Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa)imesikitishwa na uteuzi wa kamati hiyo usiozinagtia usawa wa kijinsia.

Katika taarifa ya Tamwa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Rose Ruben ilieleza kusikitishwa kwake na kamati ya kutafuta vazi hilo na kuratibu zote kwa pamoja zenye wajumbe zaidi ya 10 zikiwa na wanawake wawili pekee mbunifu wa mitindo Hadija Mwanamboka na mtangazaji Fatuma Hassan, maarufu DJ Fetty.

“Si kwamba tunakosoa weledi wa kamati zilizoteuliwa, ila Tamwa ina wajibu wa kutetea ushiriki wa wanawake katika uongozi na maamuzi”alisema sehemu ya taarifa hiyo.

Advertisement