Kifo cha Biz Markie kilivyoanza na tetesi

Ni mshumaa uliozima ghafla, hivyo ndivyo inavyoweza kuelezwa baada ya Julai 16, 2021 kutangazwa rasmi kifo cha mmoja kati ya marapa mashuhuri Marekani, Marcel Hall.
Rapa huyu kisanii alikuwa anatambulika kwa jina la Biz Markie.
Kifo chake kinaelezwa kilisababishwa na kuugua kisukari kwa muda mfupi.
Tetesi juu ya kifo chake zilianza Julai mosi mwaka huo baada ya baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii katangaza kifo chake.
Hata hivyo, mmoja kati ya wawakilishi wake walikanusha taarifa hizo na kudai ni mgonjwa na yuko katika uangalizi wa madaktari bingwa.
Ilipofika Julai 16 umma ulitaarifiwa rasmi juu ya kifo cha nguli huyo katika Hospitali ya Baltimore, alifariki akiwa na umri wa miaka 57.
Alizikwa katika makaburi ya ya Pinelawn Memorial Park mjini New York.
Msiba wake uligusa mioyo ya watu wengi, wakiwamo mashabiki na hata viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa, hali iliyowafanya kutuma salamu za rambirambi kwa familia.
Baadhi ya viongozi hao ni aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama pamoja na mkewe.
Marcel katika kipindi cha uhai wake aliwahi kutoa nyimbo zilizofanya vizuri kitaifa na kimataifa, ikiwamo Just a Friend ambayo iliingia katika nyimbo 100 bora za hip hop.