Kimewaka, Harmonize kuwaburuza mahakamani waliomchafua

Wednesday April 14 2021
harmo pic
By Clezencia Tryphone

HATIMAYE msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmonize ameibuka na kutolea ufafanuzi kashfa ya video inayotembea mitandaoni ikidaiwa ni muhusika ni yeye.

Karibuni katika mtandao wa Instagram kumekuwepo na sintofahamu juu ya msanii huyo akishutumiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa mpenzi wake Kalaja Masanja ajulikanaye kwa jina la Paula akidaiwa kumtumia picha za utupu.

Masaa mawili yaliyopita kupitia Instagram, Harmonize ameandika kuwa sakata lililokuwa likiendelea juu yake katika mitandao ya kijamii lina lengo la kumchafua yeye na brand yake aliyoitengeneza kwa kutumia pesa nyingi.

Harmonize ameandika, "Video zilizotengenezwa na kusambazwa mitandaoni zikiwa zinaonyesha sura yangu na kuunganishwa na utupu wa mtu mwingine kisha kuunganishwa na sauti yangu kwa lengo la kunichafua kunidhalilisha na kuharibu brand yangu,"

"Brand ambayo nimeitengeneza kwa mabilioni ya shilingi, itoshe tu kusema moja sio mimi, narudia sio mimi na sina maumbile yale, 2 hiyo video ninayoongea na mtu nikiwa bafuni nilikuwa naongea na mtu niliekuwaga nae katika mahusiano ni kawaida mtu kuzungumza na mtu wako,"

"Wakati wowote mahala popote sitaki kujua aliyetengeneza ni nani au kaipataje ila ninachosema ni kwamba yeyote aliyehusika na hili sawala linalolenga kunichafua na kunizalilisha lazima narudia lazima atafikishwa mahakamani ili kukomesha chuki na tamaa zinazo athiri watu wasiokuwa na hatia," amesisitiza.

Advertisement

Aidha Harmonize amedai kupitia wakili wake atawashitaki watu wanaotumia akaunti ya Baby_udaku, Rayvanny, Officialbabalevo, Divatheebawse, Jumalokole2, Bongotrending_habari, Bintikigoma na ningine nyingi zilizopost video hiyo katika instagram.

"Hiyo ni orodha fupi ya majina ya watu ambao pengine hutowaona tena hapa instagram watanilipa fine kubwa ikiambatana na kifungo juu ili iwe mwiko kama sio mfano maana sheria itafwata mkondo jopo la wanasheria wangu wapo kazini," amesema Harmonize.

Advertisement