Lil Nas, wasanii nyota wasisimua na mavazi ya kipekee

Nyota wa muziki wa rap, Lil Nas
Muktasari:
- Nyota wa muziki wa rap, Lil Nas jana alivalia nguo tatu tofauti alizozionyesha wakati akiingia katika tamasha la MET Gala, ambalo lilijumuisha wasanii wengine nyota wa Marekani wakionyesha mavazi ya kipekee.
New York, Marekani (AFP)
Nyota wa muziki wa rap, Lil Nas jana alivalia nguo tatu tofauti alizozionyesha wakati akiingia katika tamasha la MET Gala, ambalo lilijumuisha wasanii wengine nyota wa Marekani wakionyesha mavazi ya kipekee.
Tamasha hilo, ambalo pia hujulikana kama Met Ball na ambalo jana lilifanyika katika ukumbi wa Metropolitan Museum Art, hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia taasisi ya makumbusho ya sanaa ya mavazi ya jijini New York.
Umati wa watu 400-- wote wakiwa wamepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19-- uliojumuisha wacheza filamu, wanamichezo, wanamuziki, washairi na watumbuizaji ulihudhuria tamasha hilo, wengi wao wakiwa hawajavaa barakoa tofauti na miongozo ya kidunia kukabili ugonjwa huo uliosababisha gala hilo lisiwepo mwaka jana.
Lil Nas, aliyevalia mavazi yaliyobuniwa na Donatella Versace, alisisimua watu kutokana na muonekano tofauti kila alipovua vazi moja.
Kwanza, Lil Nas alivalia vazi mithili ya joho lenye michirizi ya dhahabu, likiwa na muonekano wa kifalme. Lilikuwa na mkia mrefu na hivyo kusababisha macho ya wengi kuvutwa, hiyo ikiwa ni siku chache baada ya rapa huyo kuvalia vazi ambalo ni nusu suti-nusu gauni katika tamasha la VMAs.
Baada ya kupiga picha kadhaa kwenye zuria jekundu, Lil Nas alivua joho hilo la kifalme na hivyo kubakia na suti ya dhahabu inayomeremeta, ikiwa na umbile kama robbot. Na muda mfupi baadaye, suti hiyo ikavuliwa na wapambe wake kwa kuvutwa mithili ya kuichana na hivyo kubakia na vazi linalofuata mwili lililo na nakshi maarufu za mbunifu wake wa mavazi, Versace.
Ilikuwa ni siku ya kumaliza kila kitu kwa wasanii wakubwa duniani, huku Lil Nas akihudhuria tamasha hilo kwa mara ya kwanza. Waliofunga awamu hiyo ya kutamba kwa mavazi walikuwa Rihanna na mpenzi wake ASAP Rocky, ambao walichelewa kuingia.
Kama tetesi lilivyokuwa msanii huyo wa muziki, mjasiriamali na anayeabudiwa katika tamasha hilo la MET, aliwasili akiwa amevalia nguo iliyobuniwa na Balenciaga; gauni kubwa la rangi nyeusi kama la malkia, huku nkola yake ikisimama kuizunguka shingo. Vazi hilo ni sehemu ya mavazi ya kampuni hiyo ya Kifaransa ambayo inarejea katika maonyesho ya mavazi baada ya miaka 53, ikiongozwa na Demna Gvasalia.
"Ni halisi," alisema rapa wa Marekani, Megan Thee Stallion, ambaye alihudhuria tamasha hilo kwa mara ya kwanza na aliyevalia vazi lililobuniwa na Coach.
Mwimbaji Frank Ocean aliingia na nywele za kijani na akiwa amebeba kitu ambacho watumiaji wa Twitter hukiita "robot baby" huku akiwa amevalia vazi linalometameta la rangi ya shaba na nyeusi lililobuniwa na Simone Biles. Aliweza kukanyaga mguu moja kwenye ngazi moja na hivyo kuhitaji watu sita kumsaidia kumnyanyua.