Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Vanessa Mdee na Rotimi

Saturday September 11 2021
mambo10pic
By Peter Akaro

Dar es Salaam. Siku chache zilizopita msanii wa Bongofleva, Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi waliweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza toka wachumbiane Desemba 2020.

 Wawili hao wanaishi nchini Marekani, tayari Vee Money ametangaza kuachana muziki, huko Rotimi mwenye asili ya Nigeria akiendelea na muziki pamoja uingizaji wa filamu.

Haya ni mambo 10 ambayo pengine wewe au rafiki yako hayafahamu kuhusu wapenzi hao ambao kwa sasa wanagonga vichwa vya habari na kuteka mazungumzo mtandaoni. Karibu.

1. Kwa mara ya kwanza walikutana Julai 2019 kwenye Tamasha la Essance Festival nchini Marekani ambapo wote walitumbuiza kwa wakati tofauti na jukwaa tofauti pia kutokana na mpangilio ulivyokuwa.

2. Vanessa na Rotimi wamezaliwa mwaka mmoja (1988) ila Bibie kamzidi Mshikaji, Vee amezaliwa Juni 7, 1988 Arusha, Tanzania, huku Rotimi akiwa amezaliwa Novemba 30, 1988, New Jersey, Marekani.

3. Siku ambayo wanakutana Vee alikuwa na mdogo wake, Mimi Mars, na siku hiyo hiyo ndipo walibadilisha na namba za simu na kuanza kuwasiliana ingawa utofauti masaa kati yao ilikuwa changamoto hapo awali.

Advertisement

4. Kwa mujibu wa Vanessa, ilimchukua siku mbili pekee kutambua kuwa Rotimi ni mwanaume ambaye atakuwa naye maisha yake, hiyo ni baada ya kwenda mapumziko pamoja ambapo walizima simu kwa kipindi chote.

5. Kipindi Romiti anakaribia kuanza kushuti filamu ya Come to America 2, aliambatana na Vanessa hadi studio za Tyler Pery ambazo ni maarufu duniani kwa uzalishaji wa filamu.

6. Kabla ya kukutana, Vee alikuwa anafahamu zaidi nyimbo za Rotimi lakini upande wa filamu sio sana, ni mara chache aliweza kuangalia tamthilia ya Power iliyompa umaarufu zaidi Rotimi.

7.Vitu anavyoweza kufanya vizuri Vanessa maishani ni Muziki na Utangazaji wa TV na Radio, wakati upande wa Rotimi ni Muziki, Uigizaji na Mitindo.

8. Kwa mujibu Vee mwenyewe, Rotimi anampenda sana Mungu, ni mkarimu, anapenda watu, anaejilewa, ajitambua, ana hekima na  huwezi kumdanganya kitu chochote kile.

9. Vanessa ametokea kwenye video ya wimbo wa Rotimi 'Somebody' ikiwa ndio kazi ya kwanza ya kisanaa kufanya pamoja, hata hivyo Vee alitokea kwenye video ya wimbo wa aliyekuwa mpenzi wake, Jux 'Sisikii', ikiwa pia ndio kazi ya kwanza kufanya moja pia.

10. Wawili hawa ni wasomi wa Chuo Kikuu, Rotimi ni msomi wa Bachelor Degree upande Communication toka Nothwestern University nchini Marekani, Vanessa Mdee akisomea Law toka Catholic University of Easterm Africa nchini Kenya. 

Advertisement