Mfahamu Hiba Abouk mtalaka wa Hakimi

Mwigizaji Hiba Abouk. Picha na mtandao

Muktasari:

  • Abouk, Hakimi waliingia kwenye ndoa mwaka 2020 na kufanikiwa kupata watoto wawili wa kiume kabla ya kutenga mwaka huu.

Dar es Salaam. Hiba Abouk aliyeachana na mumewe Achraf Hakimi, ni mwigizaji wa Uhispania ambaye aliomba talaka baada ya aliyekuwa mumewe kushtakiwa kwa kujaribu kumbaka mwanamke wa miaka 24.

Abouk (36) alizaliwa Madrid, Uhispania ana asili ya Tunisia na Lybia pia ni mtoto wa mwisho kati ya watoto wanne wa familia ya Abouk.

Muigizaji huyo ambaye amejipatia zaidi umaarufu katika kipindi chake cha El Principe kinachorushwa katika moja ya runinga nchini Uhispania.

Achraf Hakimi akiwa na aliyekuwa mke wake Hiba Abouk. Picha na mtandao

Pia Abouk ni mwanamitindo nyota. Mwaka 2014 alitambuliwa kama mwanamke mrembo katika Tuzo za Cosmotalian Beauty.

Abouk na aliyekuwa mumewe Hakimi walifunga ndoa mwaka 2020 na kufanikiwa kupata watoto wa kiume wawili, Amin na Naim.

Inaelezwa Abouk ana utajiri wa Dola milioni 2 sawa na Sh4.6 bilioni na endapo Hakimi angekuwa na mali angepokea Dola milioni 8.5 sawa na Sh18.7 bilioni kama ombi lake la kugawana mali na mtalaka wake huyo.

Abouk, ambaye amemzidi miaka 12 Hakimi, utajiri wake unatokana na kazi yake ya uigizaji na matangazo na vipindi vinavyoruka kwenye runinga.

Hakimi (24) ana utajiri wa Dola milioni 24, sawa na Sh56.2 bilioni ingawa asilimia 80 ya mshahara wake anaolipwa kwa mwezi unaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya mama yake.


Imeandaliwa na Emmanuel Msabaha.