Msanii Rwanda afariki akiwa mahabusu

Thursday September 02 2021
Jay pc
By Anna Potinus

Kigali. Msanii maarufu nchini Rwanda, Jay Polly amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu hospitalini jijini Kigali.


Jay aliugua gafla akiwa mahabusu akisubiri kusikilizwa kwa kesi ya matumizi ya dawa za kulevya iliyokuwa ikimkabili.


Kaka wa marehemu, Maurice Uwera amesema walipokea taarifa za kifo bila kupatiwa maelezo ya kutosha ya namna kilivyotokea.
Hadi sasa mamlaka husika haijasema chochote kuhusiana na chanzoi cha kifo hicho.


Mashabiki mbalimbali wa msanii huyo wameonyesha walivyosikitishwa na kifo hicho na wamekuwa wakituma salamu za pole kupitia mitandao yao ya kijamii.

Advertisement