Mwanamuziki Hussein Jumbe afariki dunia

Mwanamuziki Hussein Jumbe enzi za uhai wake.

Dar es Salaam. Msiba mkubwa kwa wanamuziki wa dansi.  Mwanamuziki maarufu wa dansi, Hussein Jumbe amefariki dunia.

Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound,  amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Habari ambazo Mwananchi zimetufikia hivi punde, Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Twangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.


Endelea kufatilia Mwananchi na mitandao yake kwa taarifa zaidi.