Mwanamuziki mkongwe, Father Kidevu afariki dunia

Muktasari:

  • Father Kidevu aliyekuwa mpiga kinanda na vyombo vingine, alifanya kazi na bendi mbalimbali zikiwamao Bima Lee Orchestra, Biashara Jazz, Tancut Almas na Washirika (Watunjatanjata), kabla ya kuunda bendi yake iliyoitwa Hisia Sound.

Dar es Salaam. Mwanamuziki mkongwe wa dansi, Abdul Salvador maarufu kwa jina la Father Kidevu amefariki dunia jana alasiri Novemba 2 baada ya kulazwa katika hospitali ya Amana jijini hapa akipatiwa matibabu.

 Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 3, mwanamuziki waliofanya kazi pamoja, John Kitime amesema Father Kidevu atazikwa leo Novemba 3 katika makaburi ya Karume Dar es Salaam.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba atazikwa Karume nyuma ya soko la Machinga ambako ni karibu na nyumbani kwao,” amesema.

Father Kidevu aliyekuwa mpiga kinanda na vyombo vingine, alifanya kazi na bendi mbalimbali zikiwamao Bima Lee Orchestra, Biashara Jazz, Tancut Almas na Washirika (Watunjatanjata), kabla ya kuunda bendi yake iliyoitwa Hisia Sound.

“Alikuwa akipiga muziki wake hapa, baadaye akaenda Uarabuni na Norway,” amesema Kitime.