Prince Harry, J-Lo wajumuika tamasha la Los Angeles

Monday May 03 2021
Jlo pc
By AFP

Los Angeles, Uingereza. Prince Harry wa Uingereza ameungana na nyota wa muziki a pop, akiwemo Jennifer Lopez katika tamasha lililojaa wasanii nyota jijini Los Angeles jana Jumapili, kushauri chanjo iharakishwe na kutolewa kwa usawa duniani, wakati akipaza sauti kusaidia India ambako ugonjwa wa virusi vya corona umepamba moto.

Tamasha hilo linaloitwa "Vax Live: The Concert To Reunite The World" lilijumuisha ujumbe kutoka kwa Papa na Rais Joe Biden na kuwepo kwa wacheza filamu nyota wa Hollywood kama Ben Affleck na Sean Penn.

Tamasha hilo litarushwa katika televisheni na YouTube Mei 8, baada ya kurekodiwa mbele ya maelfu ya watu waliokamilisha chanjo kwenye uwanja wa michezo California.

"Usiku wa leo, tunashikamana na mamilioni ya familia nchini  India, ambako kuna wimbi la kutisha la pili," alisema Prince Harry, ambaye alipokewa kwa watu kuonyesha heshima ya kusimama.

"Virusi haviheshimu mipaka, na kupata chanjo hakuwezi kuamuliwa na jiografia," aliongeza Harry, akionekana kwa mara ya kwanza katika hadhara kubwa jimboni California tangu ahamie Marekani mwaka jana pamoja na mkewe, Meghan Markle, ambaye hakuwepo.

Tamasha hilo liliandaliwa na Global Citizen, taasisi ya kimataifa ya harakati, likilenga kupambana na upotoshaji wa chanjo huku likitoa wito kwa viongozi duniani na mashirika kuchukua hatua na kutoa michango.

Advertisement

Maelfu ya mashabiki walikusanyika ndani ya uwanja mkubwa ambao ujenzi wake ulikamilika hivi karibuni wa SoFi jijini Los Angeles, ikiw ani mara ya kwanza kwa mkusanyiko kama huo. Wahudhuriaji wengi walikuwa ni wafanyakazi wa afya waliomstari wa mbele, baadhi wakivalia sare za manesi na madaktari.

jlo pcc

Selena Gomez ndiye aliyeendesha tamasha hilo, linalotaka dozi na fedha ziende katika nchi masikini duniani hata wakati California na sehemu nyingine za Magharibi zikiwa zimetoka kufungia watu majumbani kudhibiti maambukizi, lakini masharti yamelegezwa baada ya chanjo.

Naye J-Lo aliwaambia mashabiki kuwa alilazimika kusherehekea Krismasi bila ya mama yake kwa mara ya kwanza kutokana na janga la corona-- kabla ya kumpandisha mama huyo kuimba "Sweet Caroline".

Advertisement