Rapa A$AP Rocky, Rihanna wapenzi rasmi

Thursday May 20 2021
Riahana pc

Kumekuwepo na hisia kuwa rapa A$AP Rocky na Rihanna ni apenzi, lakini hilo halina budi kuachwa. Sasa nyota huyo wa rap amethibitisha.


Rapa huyo ameweka bayana kwamba Rihana "ni mpenzi wa maisha yake" wakati alipohojiwa na GQ kuhusu mwanamuziki huyo ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.


Uvumi kuhusu mahusiano yao ulianza mapema mwaka 2013 wakati A$AP Rock alipomsaidia Rihana katika ziara yake ya maonyesho ya muziki aliyoiita Diamonds World Tour.


"Inawezekana analingana na mamilioni ya wengine. Nadhani unapojua, unajua," alisema akikaririwa na shirika la utangazaji la BBC. "Ndiye anayefaa."


Mbali na kumsaidia ziara ya Diamond World Tour, rapa huyo alionekana kuanza kumfuatilia tangu mwaka 2012, wakati alipoungana naye kutumbuiza wimbo wa "Cockiness (Remix) katika tamasha la kutuza wasanii la MTV VMA na kuwa naye nyuma ya jukwaa.


Desemba mwaka 2019, walitembea pamoja juu ya zuria jekundu katika tamasha la tuzo za maonyesho ya mavazi la Uingereza — na wakatumia muda mwingi zaidi pamoja baada ya Rihanna kutengana na Hassan Jameel mwezi uliofuatia.

Advertisement


Tangu wawe wapenzi rasmi, wanaepuka kupigwa picha wakiwa pamoja.


BBC imeandika kuwa rapa huyo anasema mpenzi wake amechangia kwa kiasi kikubwa katika albamu yake mpya, ambayo pia inamshirikisha Morrissey.


Alipoulizwa anajisikiaje kuwa katika uhusiano, rapa huyo alijibu "vizuri zaidi. Vizuri zaidi sana wakati unapompata mtu."


Rocky pia alizungumzia suala la kwenda naye nchini kwao Barbados mwaka jana wakati wa Krismasi, na kuhusu asili yake katika kisiwa hicho ambako baba yake alitokea na kuhamia Marekani.


"Ilikuwa ni kama kurejea nyumbani," amesema Rocky akikaririwa na yahooentertainment.com.


"Ilikuwa safi. Kila mara nilikuwa nawaza itakuwaje kwa baba yangu. Na nilitembelea maeneo hayo, na amini usiamini, ilikuwa raha. Ni ugenini lakini kumezoeleka."

Advertisement