Rayvanny aanza kushusha madude chini ya lebo yake

Wednesday April 07 2021
rayvannpic
By Nasra Abdallah

Msanii Raymond Mwakyusa maarufu kwa jina la Rayvanny ameanza kuachia video za nyimbo akiwa kwenye lebo yake ya Next level Music.

Lebo hiyo aliizindua rasmi Machi 10, 2021 na kuwa msanii wa pili kufungua lebo yake akiwa anatokea lebo ya Wasafi, akitanguliwa na msanii Harmonize.

Rayvanny leo Juamanne Aprili 6, 2021 ameachia video ya wimbo wa ‘Lala’ aliiomshirikisha Jux, ambao ni moja ya wimbo uliopo katika albamu yake ya ‘Sound From Afrika’.

Video hiyo ikianza inaonyesha majina ya WCB upande wa kushoto na NL Mupande wa kulia ambayo ni kifupi cha maneno ya lebo yake hiyo na hii inafanya kuwa wimbo wa kwanza kuwa na chata ya lebo hiyo kwani huko nyuma nyimbo zote zilikuwa zikiandikwa WCB.

Hata hivyo Rayvanny tofauti na Harmonize ataendelea pia kuwa chini ya WCB.

Advertisement