Rayvanny atua Songwe kunogesha ngoma za asili

Wednesday September 22 2021
Rayvanny pc
By Hawa Mathias

Mbeya. Msanii wa kizazi kipya mwenye lebo ya (WCB) Rayvanny Mwakyusa amewasili katika uwanja wa ndege wa Songwe (SIA) mkoani hapa kwa ajili ya kunogesha tamasha la ngoma za asili maarufu kama "Tulia Traditional Dance" linalotarajia kuanza kesho Septemba 23, katika uwanja vya ndege vya zamani mkoani hapa.

Rayvanny aliyepokelewa na Mwenyeji wake Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi, Meryprisca Mahundi leo Septemba 22, 2021 majira ya saa 9.15 alasiri.

Akiwasili katika uwanja huo pia amepokelewa na shamrashamra za ngoma za asili likiwepo kabila la Wasafwa ambalo ni maarufu kwa mkoa wa Mbeya.

Akizungumza mara baada ya kupokelewa msaniii huyo, amesema Mbeya ni nyumbani hivyo hatoweza kuwaangusha viongozi wa mkoa akiwepo Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliyeandaa tamasha hilo.

"Mimi Mbeya ni kwetu nilikuwa na shoo nyingine Dar es Salaam lakini nimeona hapana nije nyumbani kufanya mambo na vijana wangu wa mbeya wananijua mambo yangu lengo pia ni kitangaza utalii wa ngoma zetu za asili," amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Meryprisca Mahundi amesema kuwa Tamasha hilo la litahusisha ngomba za makabila zaizi ya 120 kutoka mikoa mbalimbali nchini na litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Waziri wa Habari Sanaa na Utamaduni Innocent Bashungwa.

Advertisement
Advertisement