Sakata baba wa Diamond lachukua sura mpya

Sunday January 17 2021
Baba Dai pic
By Nasra Abdallah

Dar es Salam. Sakata la ukweli kuhusu baba mzazi wa msanii Diamond Platnumz linaendelea kuteka masikio ya watu ambapo sasa Abdul Juma Issac anayeelezwa kuwa sio baba wa msanii huyo amekuja na jipya.

Badala ya awali kumtaka Diamond kutotumia ubini wake, mzee huyo amesema alitoa kauli hiyo kwa jazba, lakini kwa sasa hana shida ikiwa msanii huyo ataendelea kutumia jina lake.

Juzi mama wa mzazi wa msanii huyo mkali wa kibao cha Waah! Na Jeje, Sanura Kassim maarufu kwa jina la mama Dangote, alitikisa mitandao ya kijamii kwamba aliyekuwa anafamika kuwa ni baba mzazi wa msanii huyo si baba mzazi bali ni baba mlezi.

Kwa muda mrefu ilikuwa ikifahamika na wengi kwamba baba mzazi wa Diamond ni mzee Abdul Juma Issack na ndio maana msanii huyo alikuwa akitumia jina halisi la Naseeb Abdul Jumaa.

Jambo hilo lilisabababisha jana baba Diamond naye kulizungumzia na kufika hatua ya kutaka msanii huyo kuanzia sasa asitumie jina la Abdul na kuahidi kama ataendelea kulitumia atamshtaki.

Mwananchi ilimtafuta Mzee Abdul kutaka kujua kama tayari ameshaanza mchakato wowote wa kumkataza Diamond kutumia jina hilo.

Advertisement

Katika majibu yake, alisema “Sina mpango wowote wa kumchukulia sheria, kwani juzi wakati naongea na vyombo vya habari niliongea jambo hilo kwa jazba acha tu atumie, kwani hata alipolitumia alinisaidia nini mpaka leo nimkataze,”alisema Mzee Abdul.

Pamoja na hayo, alisema kiekweli kitendo alichokifnaya mama Diamond kama binadamu hajakifurahia kwani amemvua nguo mbele za watu na kueleza kwamba ameamua kumuachia Mungu ndiye muamuzi wa yote.

Je, mzee Abdu ana mamlaka ya kukataza msanii huyo asitumie jina lake.

Mwanasheria maarufu, Jebra Kambole alifafanua kwamba jambo hilo lingekuwa gumu kwa mzee huyo kutokana na ukweli kwamba Abdul ni moja ya majina ya kawaida ambalo mtu yeyote anaweza kulitumia bila ya masharti yoyote tofauti na mtu atakayeamua kutumia jina la Mwananchi Communication ambalo hili ni jina la kampuni lililosajiliwa kisheria.

“Abdul sio brand name (jina la biashara) useme kwamba angeweza kumkataza msanii huyo asilitumie, ni jina kma Nasra, Jebra, Salma nk, hivyo hata wewe kesho ukizaa mtoto wako wa kiume unaweza kumpa jina hilo na hakuna atakayekufanya lolote.

“Pia ni jina ambalo huwezi kulisajili katika hakimiliki, hivyo baba Diamond hata angefanya nini asingeweza kukataza jina hilo lisitumike labda mpaka hapo Diamond mwenyewe atakapoamua vinginevyo,”alisema Kambole.

Wakati kuhusu Diamond kama atataka kubadili jina, Kambole alisema ana nafasi hiyo kwa kutumia nyaraka inayoitwa hati ya kubadili jina.

“Nyaraka hii Diamond atapaswa kwenda kwa mwanasheria kutengeneza nyaraka hiyo na kisha kuipelaka kwa msajili wa nyaraka..

Hata hivyo alipoulizwa kama haiwezi kumuathiri msanii huyo katika shughuli zake za kibiashara, alisema hakuna kitu kama hicho kwani jina la kibiashara analolitumia ni Diamond Platnumz na sio Naseeb Abdul.

Ushauri wake kwa baba Diamond kama anataka kujua ukweli kuhusu mtoto ni wa nani, njia rahisi na ya uhakika ni kupima vinasaba.

baba dai pic 2

“Sasa hivi hakuna uthibitisho wowote kuwa Diamond ni mtoto wa nani zaidi watabaki kuongea tu lakini uthibitisho wa kisayansi wa DNA ndio utatoa ukweli wa yote haya kama wahusika watakuwa tayari lakini,”alisema Kambole.


Mama Diamond aeleza sababu ya kumpa Diamond jina la Naseeb Abdul

Akieleza sababu ya kumpa jina la Naseeeb Abdul badala ya Naseeb Salim Nyange baba ambaye mama Diamond anaeleza kuwa ndio mzazi, mama huyo alisema ni kutokana na siku aliyokwenda kujifungua mzee Abdul ndiye aliyempeleka hospitali.

Maneno haya bado yanawachanganya watu ukizingatia kwamba mama huyu alishasema mzee Abdul ambaye ni baba mlezi kuwa alikataa mimba ya msanii huyo na hakuwa na msaada wowote katika makuzi yake..

Advertisement