Sakata la Mfaume, Msangi lazidi kunoga, TPBRC yawatolea nje

Monday April 12 2021
mfaume pic
By Imani Makongoro

Sakata la bondia Mfaume Mfaume kudai kudhulumiwa kwenye pambano lake la Russia hivi karibuni limechukua sura mpya baada ya promota wa ngumi Jay Msangi kutaka bondia huyo achukuliwe hatua na Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC).

Mfaume alichapwa na mwenyeji, Rizvan Elikhanov,kwa Technical Knock Out (TKO) raundi ya pili ya pambano lililokuwa la raundi nane ambalo liliibua sintofahamu baada ya Mfaume kudai kukatwa asilimia 80 ya malipo ya pambano hilo.

Mfaume alidai kupewa taarifa hizo na wakala aliyeambatana naye nchini Russia saa chache baada ya pambano hilo, huku akidai pambano hilo lilikuwa na 'figisu' nyingi.

Hata hivyo, Msangi ambaye ndiye wakala aliyetafuta pambano hilo alidai Mfaume na bondia mwingine Mtanzania, Maono Ally walikatwa pesa za malipo kutokana na kucheza chini ya kiwango.

"Ilikuwa wasilipwe kabisa, mimi ndiye nilizungumza na promota akasema anawakata dola 1000 kila mmoja, hivyo Mfaume akabakiwa na Milioni 6, tofauti na alivyodai kwamba amerudi na Milioni tatu,".

Amedai kupeleka suala lao TPBRC ili kupata suluhu na wamewaita yeye Msangi na Mfaume katika kikao kitakachofanyika baadae leo.

Advertisement

Hata hivyo, kaimu rais wa TPBRC, Agapeter 'Mnazareth' Basil amekataa kulifahamu sakata hilo.

"Halijafika mezani kwetu wala sijasikia taarifa hizo," amesema Agapeter.

Advertisement