Sauti za Busara kutangazwa mubashara Afrika

Sauti za Busara to broadcast live across Africa

Muktasari:

  • Baada ya kutumbuiza mubashara na kuleta shamrashamra katika viunga vya Mji Mkongwe, Zanzibar tangu ilipoanzishwa  2004,  mwaka huu tamasha litaoineshwa mubashara barani Afrika kupitia Plus TV kwenye kisimbuzi cha DStv’s Channeli 294.

Zanzibar. Maandalizi ya tamasha kubwa la Sauti za Busara2021 zinaendelea na waandaaji wanaamini kwamba watatoa burudani la kukata na shoka na kukumbukwa.

Baada ya kutumbuiza mubashara na kuleta shamrashamra katika viunga vya Mji Mkongwe, Zanzibar tangu ilipoanzishwa  2004,  mwaka huu tamasha litaoineshwa mubashara barani Afrika kupitia Plus TV kwenye kisimbuzi cha DStv’s Channeli 294.

Akizungumzia maandalizi hayo, mkurugenzi wa tamasha Yusuf Mahmoud alisema mipango imefanywa kuwawezesha wapenzi wa tamasha ambao wanakabiliwa na shida katika kusafiri kufurahiya tamasha hiyo wakiwa sebuleni kwao.

"Tunafurahi juu ya ushirikiano wetu na Plus TV ambayo inatangaza kwenye DSTV Channeli 294 na tuna hakika hii itawezesha watazamaji kufurahiya sifa za kipekee za tamasha hii na Zanzibar kwa ujumla," alisema ndugu Mahmoud.

Aliongeza kuwa licha ya kupunguza idadi ya siku hadi mbili tofauti na nne zilizozoeleka, tamasha hilo litakuwa la ubora wa hali ya juu, na jukwa kuu litakuwa ndani ya Ngome Kongwe.

Kati tarehe 12 na 13 Februari 2021, kuta za Mji Mkongwe, Zanzibar zitatetemeka tena kwa sauti za muziki wa Kiafrika, vikundi tisa vikiwakilisha Tanzania na nne zaidi kutoka Bara lote la Afrika.

Kama kawaida, tutaendelea kuangaza vipagi vinavyoibuka.  Miongoni mwa makundi hayo wapo: 

YugenBlakrok (Afrika Kusini), MorenaLeraba (Lesotho), Barnaba Classic (Tanzania), DullaMakabila (Tanzania), Djam (Algeria), Siti Muharam (Zanzibar),Sandra Nankoma (Uganda), Stone Town Rockerz (Zanzibar), Richie Lumambo (Tanzania) na wengine kadha.