Sintofahamu Diamond kununua gari la kifahari

Friday June 04 2021
DIAMONDPIC

Nillan, mtoto wa mkali huyo wa wimbo wa Waah

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Inaelezwa kuwa msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz amenunua gari jipya la  kifahari aina ya Cadillac Escalade Sky Captain.

Nillan, mtoto wa mkali huyo wa wimbo wa Waah aliomshirikisha mwanamuziki wa DRC Congo, Koffi Olomide ameonekana ndani ya gari hilo.

Katika ujumbe uliowekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa mtoto huyo ambaye amewasili nchini hivi karibuni na mama yake, Zari akitoka Afrika Kusini, unaashiria kuwa Diamond ndiye mmiliki  wa gari hilo ingawa mwenyewe wala uongozi wake hawajathibitisha hilo.

Gari hilo toleo la 2016, ndani kuna friji ya kuhifadhi vinywaji na matunda, pia ina mfumo unaoweza kugundua hali ya hewa kulingana na eneo lililopo  na kuna televisheni ya inchi  48.
Katika orodha ya magari saba ya starehe duniani linashika nafasi ya tano. Ili kununua gari hilo mfukoni unatakiwa kuwa na kati ya Dola 350,000 hadi 500,000 za Marekani (Sh811 milioni hadi Sh1.15 bilioni).

Imeandikwa na

Peter Akaro, Mwananchi

[email protected]

 

Advertisement
Advertisement