Snoop Dogg kuachia albamu ya 18

Sunday April 04 2021
snoop pc

Rapa Snoop Dogg ametangaza ujio wa albamu yake mpya iitwayo “From Tha Streets 2 Tha Suites” ambayo itakuwa ya 18.

Wimbo wa kwanza katika albamu hiyo uitwao “Roaches in My Ashtray” aliuachia jana Aprili 2.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, rapa huyo aliandika kuwa ataachia albamu hiyo hivi karibuni.

Mara ya mwisho rapa huyo kutoa albamu ilikuwa mwaka 2019 iliyokuwa inakwenda kwa jina la “I Wanna Thank Me”.

Advertisement