Tamasha la Oscars sasa kama filamu

Monday April 19 2021
oscar pc

Sherehe za kutuza wasanii a filamu za Oscars zimebadiklishwa muundo na kuzipa ladha ya filamu, zikitoa muda zaidi kwa washindi kuzungumza, wakati barakoa za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona zikichukua nafasi kubwa, watayarishaji wa tamasha hilo walisema Jumamosi.


Janga la corona na watayarishaji wapta watatu wamesababisha kufanyika kwa ubunifu huo, ambao umeondoka na tamasha lililozoeleka ambako wasanii wakubwa duniani wa filamu hukabidhiwa tuzo za Oscars mbele ya umati wa watu maarufu zaidi ya 4,000 waliokaa kwenye viti, ukijumuisha wasanii wa kada ya juu na maofisa.


Badala yake, sehemu kubwa ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 25 itafanyika katika kituo cha Art Deco Union kilichoko Los Angeles, ambako jukwaa linajemgwa na ambako watoaji tuzo hawatafanya kazi pekee ya kufungua bahasha na kutangaza jina la mshindi.


“Halitafanana na kitu chochote ambacho kimeahi kufanyika kabla,” muongozaji filamu, Steven Soderbergh, ambaye anatayarisha onyesho hilo pamoja na Stacey Sher na Jesse Collins, alisema katika mkutano na waandishi wa habari, kwa mujibu wa AFP.

oscar pcc


Soderbergh, ambaye aliongoza filamu ya "Contagion" ya mwaka 2011, alisema janga la coeona “lilifungua fursa ya kujaribu kitu ambacho hakijawahi kujaribiwa.”
“Tunataka tamasha liwe na sauti,” alisema.

Advertisement


Soderbergh alisema sherehe hizo zitakuwa fupi kama sinema, huku watoaji tuzo wakiwa ni pamoja na Brad Pitt, Harrison Ford na Halle Berry “wakijiigiza au au angalau kuonyesha upande wao.”


Awali hotuba za washindi wa Oscar zilitakiwa kuwa za chini ya sekunde 45. Mwaka huu, Soderbergh alisema, “tunawapa nafasi. Tumewahimiza kuhadithia habari, na kusema kitu fulani binafsi.”
Watayarishaji walisema sheria kali za kujinga na maambukizi ya corona zitakuwepo, nyingi zikifuata viwango vilivyowekwa mwaka jana ili kuwezesha filamu na utayarishaji wa vipindi vya televisheni kuendelea.


Washiriki waliotajwa kuwania tuzo hizo ambao watashindwa kusafiri kwenda Los Angeles kuhudhuria sherehe hizo, watashiriki kwa njia ya satellite kutoka sehemu walipo, lakini hakuna atakayeshiriki kwa njia ya Zoom.

Advertisement