Tanasha ammwagia sifa Alikiba

Saturday October 09 2021
tanashapic
By Peter Akaro

Mwimbaji kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna amempongeza staa wa Bongofleva, Alikiba kwa kuachia albamu yake mpya 'Only One King' ambayo imetoka Oktoba 7, 2021 ikiwa na nyimbo 16.

Usiku wa kuamkia leo Alikiba alifanya listening party Nairobi nchini Kenya ambapo wasanii mbalimbali Khaligraph Jones, Otile Brown, Nyashinski na Tanasha walialikwa.

Utakumbuka Only One King ni albamu ya tatu kwa Alikiba mara baada ya kuachia Cinderella (2007) na Ali K4Real (2009).

"Ni fahari kuwa hapa, na fikiri ni albamu kali, ninatumaini Afrika na dunia nzima itaisikiliza albamu hii. Hongera, nina furaha kwa kweli kuwa hapa," amesema Tanasha Donna.

Mwaliko wa Tanasha ulipokelewa kwa hisia mseto na baadhi ya mashabiki kwa kuzingatia kuwa ni  mzazi mwenziye na Diamond Platnumz ambaye ni mshindani wa Alikiba kimuziki.

Mwaka 2015 Tanasha akiwa anafanya mitindo pekee, alitokea kwenye video ya wimbo wa Alikiba na Christian Bella 'Nagharamia'. Video hiyo ndio ilimpa umaarufu zaidi nchini Tanzania.

Advertisement

Kabla ya kuingia katika muziki, Tanasha alikuwa akifanya mitindo (Commercial Modeling) chini ya Dominique Model's Agency huko Brussels nchini Ubelgiji.

Tanasha alianza mahusiano na Diamond Desemba 2018. Akiwa na staa huyo  alianza kujikita zaidi kwenye muziki hadi akaachia  Extended Playlist (EP ) yake iitwayo ‘DonnaTella EP’ yenye nyimbo nne ambazo ni ‘La Vie’ aliomshirikisha Mbosso, ‘Gere’ akishirikiana na Diamond, ‘Ride’ aliomshirikisha msanii kutoka nyumbani kwao Kenya  Khaligraph Jones na ‘Teamo’ aliyofanya pekee yake.

Advertisement