Tupac kutunukiwa tuzo ya heshima

What you need to know:

  • Tupac Shakur kutunukiwa tuzo ya heshima kwenye Hollywood Walk of Fame, kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki duniani, Dada yake Sekyiwa ‘Set’ Shakur, anatarajiwa kupokea tuzo hiyo Juni 7, kwa niaba yake kwenye Hollywood Boulevard.

Marekani. Aliyekuwa mwanamuziki nguli wa Hip-Hop unaotambulika kama muziki wa kufoka Marehemu Tupac Shakur maarufu kama 2pac, atatunukiwa nyota ya heshima kwenye ‘Hollywood Walk of Fame,’ siku ya Jumatano Juni 7.

Kwa mujibu wa chombo cha habari, TMZ (American syndicated entertainment) wameeleza kwamba hii inakuja baada ya kupita miaka takribani 27 tangu kifo chake kitokee Septemba 13, 1996 kwa kupigwa risasi huko Las Vegas, Nevada nchini hapa.

Katika tuzo hiyo ya heshima anayotarajiwa kupewa Tupac, dada yake Sekyiwa ‘Set’ Shakur, ndie atakaepokea heshima hiyo kwa niaba ya marehemu kaka yake kwenye Hollywood Boulevard.

Heshima hii kubwa inatokana na mchango wake katika tasnia ya muziki, ambapo tukio hili litakuwa ni fursa nzuri ya kumuenzi na kuadhimisha urithi wake ulioendelea kuwa na athari kubwa katika ulimwengu wa burudani.

Miongoni mwa wageni wazungumzaji ni pamoja na Mkurugenzi Allen Hughes na Jamal Joseph, Mtayarishaji Mkuu wa filamu mpya ya Tupac inayotambulika kama ‘Dear Mama’ inayoelezea maisha ya Tupac na mama yake Afeni.

Tupac ameuza nyimbo zake zaidi ya rekodi milioni 75, katika kazi zake mbili tu, ikiwemo nyimbo ya ‘All Eyez on Me’ huku nyimbo zake zikiendelea kuchukua tuzo kubwa duniani.

Hata hivyo Tupac, atakuwa ni mwanamuziki wa tano kutokea ‘West Cost’ Pwani ya Magharibi, kutunukiwa tuzo hiyo baada ya Nipsey Hussle, Snoop Dogg, Ice Cube na Dr Dre kupata heshima hiyo.