Wasanii wa Tanzania waalikwa Kombe la Dunia 2022 Qatar

Wednesday September 29 2021
wasaniipic
By Peter Akaro

Dar es Salaam. Wasanii saba kutoka nchini Tanzania wamealikwa kushiriki katika sherehe za maandalizi ya Kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kuanza Novemba 18 hadi Desemba 18, 2022 nchini Qatar.

Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Sanaa la  Taifa (Basata), mwaliko huo umetumwa na kituo cha utamaduni kutoka nchini humo 'Qatar Cultural Village', hivyo wasanii wametakiwa kuchangamkia fursa hiyo.

Wasanii wanaoalikwa ni wa fani za uchoraji wa picha, uchoraji wa Curiculture, uchoraji wa Graffiti, uchoraji wa picha za 3D na Pantomine.

"Kufuatia fursa hiyo, Basata inawaalika wasanii wa fani hizo kujitokeza na kuwasilisha nyaraka za kazi kupitia barua pepe ya baraza [email protected] kabla ya Septemba 29, 2021," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Matiko Mniko.

Pia wasanii watakaokidhi vigezo hasa wale wanaotambuliwa na Basata watalipiwa gharama za usafiri pamoja na malazi na kituo hicho cha Qatar.


Advertisement
Advertisement