Wasanii wanaotumia lugha chafu kwenye kazi zao kikaangoni

Thursday April 29 2021
bakita pc
By Nasra Abdallah

 Dar es Salaam. Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita)  limesema litaanza kuwashughulikia wasanii wanaotumia vibaya Kiswahili katika kazi zao huku likiwatolea mfano wasanii wa Bongofleva.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Aprili 29, 2021 na mhariri lugha wa baraza hilo, Oni Sigala katika jukwaa la sanaa lililofanyika mkoani Dar es Salaam.

Sigala amesema watakuwa wakifanya kazi hiyo kwa kuandika barua na kuipeleka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ambalo jukumu lake itakuwa kutoa adhabu ikiwemo kuifungia kazi husika.

Amesema asilimia 70 ya nyimbo za Bongofleva hivi sasa zimejaa lugha za matusi na kwamba wao kama wasimamizi wa lugha hawapo tayari kuona inatumika ndivyo sivyo.

"Labda niwaambie tu wasanii kwamba Kiswahili ni bidhaa, unapoitumia na kuisambaza unapaswa kuitumia kwa usahihi na sisi ni moja ya kazi yetu kusimamia hilo ili kusiwe na upotoshaji," amesema Sigala.

Bakita cc
Advertisement

Ameongeza kuwa imefika mahali wasanii wanatumia lugha  ‘kwa kuivisha maneno ambayo ni matusi’, jambo alilodai kuwa hata watoto wanaweza kutambua.

Advertisement