Watu wapuliziwa dawa kabla ya kumuona Koffi Olomide

Sunday February 14 2021
Coffie pic
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Tahadhari ya kuepuka magonjwa ya kuambukiza imechukuliwa vilivyo kwenye onesho la mwanamuziki kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Koffie Olomide.
Show hiyo iliyopewa jina la "Mahaba ya Rhumba, imefanyika jana Jumamosi Februari  13, 2021 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Kama ambavyo serikali imekuwa ikitoa tahadhari kuchukua hatua ya kujilinda ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza, waratibu wa show hiyo waliweka mashine maalum nje ya ukumbi ambapo mtu anapita  na yenyewe kumwaga dawa.
Mwananchi ilishuhudia baadhi ya watu wakipita katika mashine hiyo ambapo uwe unatoka au unaingia dawa hiyo inakumwagigia.


Hata hivyo kuna baadhi ya watu walionekana kjkwepa dawa ile kwa kuhofia kuharibu 'make up' zao japokuwa  wasimamizi walikuwa wakali katika hilj na kujikuta wakiwarudisha baadhi kurudia kupita katika mashine hiyo.  
Ukiachilia mbali mashine hiyo pia katika milango ya kuingia ukumbini kulikuwa na watu maalum wamesimama na vitakasa mikono na kila aliyepita alimiminiwa mikononi.

Advertisement