WCB na Konde Music yupi kulamba dume kwa RC Makalla

Wednesday November 03 2021
lebo pic
By Peter Akaro

Lebo za WCB Wasafi na Konde Music Worlwide zilikuja utarabu wao wa kuomba kusimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kama mlezi wao kimuziki.

Walianza na WCB yake Diamond Platnumz ambao walimtangaza Paul Makonda kuwa mlezi wao na yeye alikuwa akijipambanua katika hilo kwa muda wote waliokuwa madarakani.

Makonda ambaya aliingoza Dar  es Salaam kuanzia  Machi 2016 hadi Julai 2020, alihudhuria  na yeye aliwaalika wasanii wa lebo hiyo katika hafla muhimu za kitaifa na hata za kifamilia.

Haikuwa ajabu pale Diamond alipomtolea wimbo 'Acha Nikae Kimya' wakati kiongozi huyo alipowekwa kiti moto mtandaoni kwa tuhuma za vyeti feki hapo mwaka 2017. Alifanya hivyo kwa vile ni mlezi wake.

Makonda alikabidhi ofisi kwa Abubakar Kunenge, lebo ya Konde Music yake Harmonize wakamwendea na kumuomba awe mlezi wao na akakubali hilo.

Kunenge ambaye sasa amehamishiwa mkoa wa Pwani, aliwahi  kufika ofisi za Konde Music na kujionea studio zake na namna wanavyofanya kazi zao na kuwapongeza kwa uwekezaji wao.

Advertisement

Kufika Mei 2021 Rais Samia Suluhu alimteua Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akichukua nafasi ya Kunenge. Miezi  kadhaa sasa Makalla yupo ndani jiji hilo lenye watu wengi nchini. Je, ni WCB au Konde Music watalamba karata ya ushindi kwa RC Makalla?. Muda ndio utaamua. 

Advertisement