Wimbo wa Harmonize, Awilo Longomba kuachiwa Aprili 23

Wednesday April 21 2021
awilopic
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Msanii wa Bongofleva, Harmonize amesema wimbo aliomshirikisha mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Awilo Longomba unaitwa Attitude na atauachia Ijumaa Aprili 23, 2021.

Ameeleza hayo leo Jumatano Aprili 21, 2021 katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii  wa Instagram akibainisha kuwa mbali na

na Awilo anayetamba na wimbo wa Rosalina, pia amemshirikisha H Baba.

Harmionize amefanya wimbo na mwanamuziki  huyo aliyepo nchini kurekodi filamu ya A life to Regret.

Awilo anayetamba pia na nyimbo za Gate le Coin, Coupe Bibamba, Porokondo, Bibala na Caroline alitua Tanzania Aprili 7, 2021 na anatarajiwa kuwepo nchini Tanzania mwezi mzima.

Advertisement