Zari atua tena Bongo na watoto wake

Tuesday June 01 2021
zari pc
By Nasra Abdallah

Zari ambaye ni mzazi mwenzie na msanii Diamond Platnumz ametua tena Bongo na watoto wake.

Mama huyo wa watoto watano ametua leo Jumanne Juni 1, 2021 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kupokelewa na mama Diamond bi Sandra  na mumewe Uncle Shamte.

Zari anakuja ikiwa imepita miezi sita tangu alipokuja tena na watoto wake, ambao ni Nillan na Latiffah, ujio ambao uliibua gumzo baada ya wawili hao(Diamond na Zari) kutengana miaka miwili iliyopita na kuwa paka na chui.

Hata hivyo kwa sasa mambo yanakwenda sawa kwani pia tayari Diamond naye Aprili mwaka huu alikwenda Afrika Kusini, kuwaona watoto wakati alipokuwa huko kwa shughuli zake za kimuziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo wa mitandao ya kijamii alieleza kuwa atakuwa nchini kwa shughuli zake za ubalozi.

Tofauti na miaka miwili iliyopita, ambapo Zari alikuwa akija nchini katia shughuli za ubalozi anafikia hotelini, safari hii amepokelewa na mama yake Diamond na kuelekea nyumbani.

Advertisement
Advertisement