Zuchu, Harmonize waachia nyimbo mpya

Friday April 23 2021
zuchupic
By Nasra Abdallah

Wasanii wa muziki wa Bongofleva, Zuhura Othuman’Zuchu’ na Harmonize, wameachia nyimbo mpya.

Wawili hao wameachia nyimbo zao hizo leo Ijumaa Aprili 22, 2021 ambapo walianza kuwajulisha ujio wake mashabiki kupitia kurasa zao kuanzia jana.

Wakati wimbo wa Harmonize ukiwa unaenda kwa jina la ‘Attitude’ ndani yake amewashirikisha mwanamuziki kutoka Jamuhuri ya Kongo, Awilo Longomba na msanii H.Baba wa Tanzania.

Zuchu wimbo wake unaitwa ‘Olakira’ akiwa amemshirikisha msanii Sere kutoka kule nchinini Nigeria.

Hii inamfanya Zuchu kufanya kazi na msanii wa pili kutoka nchini humo ikitanguliwa na ule wa ‘Nobody’ alioufanya na msanii Joeboy.

Wasanii wa Nigeria mbali ya kufanya muziki mzuri pia wamekuwa wakifanya vizuri katika anga za kimataifa ikiwemo kuongoza kuzoa tuzo kwa nchi za Afrika zikiwemo zile za Grammy walizopata hivi karibuni kwa wanamuziki wao Wizkid, Davido na Burnaboy.

Advertisement
Advertisement