Ebuana! Darassa haangalii sura

Saturday April 03 2021
darasapic
By Kelvin Kagambo

WAKATI wasanii wakubwa wakisajili wasanii wachanga wa maeneo waliyotoka kwenye lebo zao, mambo ni tofauti kwa mkali wa albamu ya Slave Become a King, Shariff Thabeet maarufu Darassa kwani kwake hasaidii msanii kwa sababu ya eneo alilotoka.

Akibonga na Mwanaspoti, Darassa alisema kwenye lebo yake ya Classic Music Group (CMG) wamesajili wasanii zaidi ya watatu lakini hakuna hata mmoja kati yao anayetokea Kiwalani, eneo ambalo Darassa anawakilisha.

“Sio kwa sababu Kiwalani hakuna wasanii, wapo lakini tunaposajili mtu hatuangalii ametoka wapi, tunaangalia uwezo,” alisema Darassa na kuongeza kuwa;

“Binafsi naendelea kusaidia wasanii wa eneo nililotoka kwa mawazo na kushikana mikono kwa staili zingine.”

Lebo ya Darassa ya CMG ilianzishwa mwaka 2016 na mpaka sasa ina wasanii wachanga wanne ambao ametangaza kutumia mwaka huu kuwasaidia zaidi.

Advertisement