Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fahamu upekee wa Uwanja wa fainali ya Euro

Fainali ya fainali za mataifa ya Ulaya (Euro) 2024 inachezwa leo kuanzia saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Olympiastadion uliopo jijini Berlin Ujerumani itakayozikutanisha England na Uhispania.

Uwanja huo una mambo matatu yanayofanya uwe na hali ya kipekee kulinganisha na vingine tisaambavyo vimetumika katika mashindano hayo.

Jambo la kwanza ni Uwanja huo kuwa pekee unaotumika kwa michezo ya fainali ya Kombe la DFB nchini Ujerumani mashindano ambayo hufanyika kila mwaka tangu 1985.

Upekee wa pili wa Uwanja huo ni historia yake ya kutopatikana kwa matokeo ya sare katika mechi zote zzilizopita za mashindano ya Euro mwaka huu ambapo kila mechi timu moja iliibuka na ushindi.

Pia katika mechi tano zilizochezwa uwanjani hapo, hakuna hata moja ambayo ilienda katika dakika 30 za nyongeza na mshindi alipatikana katika muda wa kawaida wa dakika 90.

Katika mechi ya leo ushindi kwa Uhispania utaifanya iweke rekodi ya kuwa timu iliyotwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa mashindano hayo ambapo itakuwa inafanya hivyo kwa mara ya nne.

Kwa sasa, Uhispania iko sawa na Ujerumani kileleni mwa chati ya timu zilizotwaa ubingwa wa fainali za Euro ambapo kila moja imewahi kunyanyua kombe la ubingwa mara tatu.

Hamu ya kutwaa ubingwa ni kubwa zaidi kwa England kwa vile litakuwa taji lao la kwanza la mashindano hayo kwani tangu yalipoanzishwa haijawahi kuonja ladha ya kutwaa taji la Euro.

Nuksi hiyo ya England kwenye Euro inaonekana kutoishia katika kutwaa ubingwa tu kwani hata kuingia hatua ya fainali imeingia mara moja tu hapo nyuma na hii ni mara ya pili.

Aliyepewa jukumu la kuamua shughuli ya wanaume 22 katika fainali hiyo ya leo ni refa kutoka Ufaransa, François Letexier mwenye umri wa miaka 35.

Refa huyo ambaye alianza kuwa na beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) tangu 2017, amechezesha idadi ya mechi 65 za  mashindano tofauti yaliyo chini ya Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa).

Katika fainali hizi za Euro, refa huyo amechezesha michezo mitatu, mmoja ukiwa ni wa hatua ya 16 bora na mingine miwili ni ya hatua ya makundi.

Letexier atasaidiwa na Wafaransa wenzake Cyril Mugnier na Mehdi Rahmouni huku refa wa nne akipangwa kuwa Szymon Marciniak kutoka Poland.

Marefa watakaokuwa wanasimamia teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa (VAR) ni Jérôme Brisard (Ufaransa) atakyesaidiwa na Willy Delajod (France) na watakaowapa sapoti ni Massimiliano Irrati (Italy) na Tomasz Listkiewicz (Poland).